Ijumaa, 10 Januari 2014

Mwasiti ndani ya Serebuka

Msanii wa bongo flava kutoka Tanzania House of Talent(THT)mwasiti Almasi anatarajia kutoa single yake kwa mashabiki wake inayojulikana kama Serebuka jumatatu ya januari 13 mwaka huu.

Alhamisi, 9 Januari 2014

Huyu ndiye mshindi wa African Footballer mwaka"2013"

                                       Yaya Toure wa pili kushoto



Yaya Toure(30) kutoka Ivory Coast ameibuka mshindi wa African footballer kwa mwaka 2013 Kwenye utoaji wa tuzo hii uliofanyika jana Lagos Nigeria. Mkali huyu ambae anaichezea Manchester City anajivunia kuwa mshindi wa tuzo hiyo.

Jumanne, 31 Desemba 2013

my wish in new year

namshukuru Mungu wangu wangu kwaajili ya masaa machache yaliyobakia kufikia mwaka 2014,nasema asante maana ni neema zako zilizonifanya niwe ahai mimi pamoja na familia yangu.

Nawatakia mwaka  mpya wenye mafanikio na kila lililo gumu mwaka uliopita Mungu akatengeneze njia liwe jipesi.

Happy comin new year 


Jumamosi, 28 Desemba 2013

Tips kwa mwaka mpya


Mwaka mpya unakuja kila mtu akiwa na malengo yake anayopenda Mungu amsaidie kuyatimiza. kutokana na sababu mbalimbali mtu hakuweza kutimiza maono yake kama kuwa mfanyakazi bora,kufaulu mitihani,kujenga nyumba au kuanzisha familia haijalishi vyote hivyo kama havikutimia katika mwaka uliopita sasa ni wakati wa kujipanga upya kwa mwaka ujao.Kuweka maazimio yetu,maono yetu na kumshirikisha Mungu  katika mwaka mpya wa 2014 itatusaidia kutimiza  ndoto tulizokuwa tukiota mwaka ulipita.. Tushirikiane hizi tips nne nilizopewa na rafiki yangu mpenzi miezi mitano iliyopita.

 
1. Kuanza kidogo: si vizuri kuanza kwa speed kubwa jipe muda wa kutosha ili kukamilisha kitu unachoanzisha,kuanzaa kidogo kutasaidia kujifunza taratibu na kukujengea uzoefu wa jinsi utakavyoweza kuhumudu kikubwa pindi kitakapoongezeka.Sio kukimbilia vikubwa ambavyo mwisho wa siku unalia kwa hasara au kushawishika na biashara haramu,kila kitu ni hatua kama vile mtoto anavyoanza kukaa,kutambaa,kusimama halafu hatua ya kutembea pole pole hadi mwisho wa siku ni mbio.


2. Kuwa na mlengo maalum : Unaweza kusema "Nataka kuanzisha biashara " au " Mimi nataka kupunguza uzito ," lakini unatakiwa kuweka azimio lako katika hali halisi itasaidia kweli kufikia lengo lako. Kwa mfano, jaribu kutatua kwa kujifunza jinsi ya kucheza wimbo maalum juu ya gitaa. Pia jaribu kuweka katika maandishi ili kusaiidia lengo kuwa halisi kufanyia kazi.


3. Jipe kikomo cha muda: Katika hili mtu anatakiwa ajiwekee kikomo cha kutekeleza malengo yake mfano, " Ningependa kuwa na biashara,anza kidogo kidogo utasogea lakini sio nafikiria kuanzisha biashara  siku moja hapo kamwe haitotokea,unachotakiwa ni kuchukua mara moja na kutekeleza adhima yako ya kuacha.pia na kuweka kikomo cha muda kuwa labda baada ya miezi mingapi biashara yako itakuweje.

.
4. Kuweka rekodi ya maendeleo yako: hii itakusaidia kukupa Ramani   jinsi ya kutunza azimio lako na kukufanya kufikia malengo yako.Hakuna hisia bora kuliko kuwa na lengo na kulikamilisha.Pia itakusaidia kujua wapi ulipofikia toka ulipoanza shughuli yako,iwe umeajiriwa au umejiajiri.

  

Pia tusisahau kuandika katika kumbukumbu zetu vitu tunavyotaka kuvifanya kwa mwaka mpya hii itatusaidia kutupa nguvu ya kufanya bidii katika malengo yetu na hatimaye kutimiza ndoto zetu.

Mwaka mpya mwema wenye Baraka na mafanikio,Mungu awabariki.

 

 

Jumanne, 24 Desemba 2013

Historia ya Krismas



 

Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu  ambako Wakristo husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.

 
Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii.

  • Krismasi inatokana na neno la kiingereza lenya maana "Christ`Mass" yaani misa au ibada ya Kristo kwa maana misa ya sikuu yake.

Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokelewa na lugha ya Kifaransa "noël". Hili ni mafupisho ya Kilatini natalis (dies), "(siku) ya kuzaliwa Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu Utamaduni  wa Wayahudi  wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.

Lakini baadaye Ukristo  ulienea katika Dola ya Roma na kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya Sikukuu ya Krismasi.

Tangu mwanzo wa Karne ya 3BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.

Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200.Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei wengine katika Aprili,Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.

Labda kadirio la tarehe ya 25 Desemba pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Afrikanus  tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.

samaki dili

wauzaji wa samaki wakiandaa samaki wa aina mbalimbali kwa aji;i tamasha la samaki wabichi kwa kuuzwa(Australia)katika kipindi hiki cha sherehe za krismas

Jumapili, 15 Desemba 2013

goodbye Tata Madiba



mwili wa Hayati Nelson Mandela kijijini Qunu


Mwili wa hayati Nelson Mandela umepelekwa katika mkoa wa Eastern Cape kwa safari ya mwisho kabla ya kuzikwa siku ya Jumapili kijijini Qunu.

Idadi kubwa ya watu walifurika barabara angalau kumtupia jicho shujaa wao na kutoa heshima zao za mwisho.

Taarifa zinazohusiana

Nelson Mandela

Mandela aliyefariki tarehe tano Disemba atafanyiwa maziko ya kitaifa siku ya Jumapili,

Takriban watu 100,000 walitoa heshima zao za mwisho kwa Mandela mjini Pretoria siku ya Ijumaa kabla ya mamia ya wengine kukosa fursa hiyo pale walipokatazwa kumuona Mandela kutokana na ufupi wa mda.

Kijiji cha Qunu

Kijiji cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson Mandela, kinaomboleza kifo cha shujaa aliyetoka katika kijiji hicho Nelson Mandela.

Mazingira hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki.

Visima vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka hawezi kuviona sasa. Lakini viwanja vya kijiji hiki viko chini ya majabali ambayo yeye na rafiki zake walikesha wakichezea.

Ni viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua asali misituni na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo.

Alipokuwa na umri wa miaka 5, Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu safari yake alivyopigania uhuru wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga Ng’ombe, na kupitia kwa kazi hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya watu wa kabila la AbaTembu na Ng’ombe wao.

Alisomea hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa huzuni wakati alimzika babake kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka 1990 alipokuja kutembelea kaburi la mamake , alisema aliona umasikini mkubwa machoni mwa watu wa Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa takataka kitu ambacho hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.

Hata hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka kimebadilika pakubwa, ni kisafi kikubwa na kina dalili za maendeleo, wala sio taswira aliyoitoa Mandela katika kumbukumbu zake kuhusu nyumbani.

Na sababu moja ya hilo ni kuwa alijenga nyumba hapa pamoja na shule, alilemaji, umeme, pamoja na mapato kwa watu wa eneo hili kutokana na makavazi aliyojengewa Mandela ambako atazikwa.

 

Jumatatu, 9 Desemba 2013

Shughuli ya mazishi ya marehemu Tabu Ley Rochereau gwiji wa Rumba Afrika

Viongozi wa serikali ya DRC wamehudhuria mazishi hayo huku waakilishi kutoka nchi jirani ya Congo Brazaville pia wamehudhuria mazishi hayo.

Tabu Ley alifariki mwezi Novemba akiwa na umri wa miaka 76 akipokea matibabu nchini Ubelgiji.

Wengi walimkumbuka Tabu Ley kwa mziki wake na kwa talanta yake kwa utunzi wa nyimbo zake zilizowagusa watu wengi Afrika. Tabu Ley amefanyiwa mazishi ya kitaifa

Mwanamziki huyo ambaye pia alikuwa mwanasiasa, hakuwahi kupona tangu alipougua kiharusi mwaka 2008 na hali yake iliendelea kuwa mbaya hadi alipofariki Novemba 30.

Alizaliwa mwaka 1937 katika kijiji kimoja kidogo Magharibi mwa mkoa wa Bandundu, na hapo ndipo nyota yake ilianza kung'aa a katika fani ya muziki wa Rumba mapema miaka ya sitini.

Baadhi ya nyimbo alizoimba zilikuwa Adios Thethe na Mokolo nakokufa, na zilisaidia katika kufanya mziki wa Rumba kupendwa sana.

Tabu Lei alitaka sana kuwa waziri wa utamaduni katika serikali ya Laurent-Desire Kabila --babake rais Joseph Kabila, lakini badala yake akawa naibu gavana wa mji wa Kinshasa.

Alikimbilia usalama wake wakati wa utawala wa aliyekuwa rais Mobutu Sese Seko kati ya mwaka 1965 to 1997, na mnamo mwaka 1990, serikali ya Mobutu ikapiga marufu album yake Trop, c'est trop.

 

Tanzania ya leo


Tanzania imetimiza miaka 52 toka ipate uhuru wake kutoka kwa waingereza walioyoitawala Tanganyika kama ilivyokuwa inajulikana wakati huu  kuanzia mwaka 1918-1961.
Ikiwa ni miaka 52 ya nchi yetu kujitawala yenyewe nashuhudia mambo mbalimbali yanayoonyesha maendeleo japo tupo katika orodha ya nchini zinazoendelea Dunia.
Maendeleo ni hali ya kutoka katika hali duni kuelekea katika hali ambayo ni nzuri iwe kiuchumi,kisiasa na utamaduni.
Wakati tunapata uhuru 1961 nchi yetu ilikuwa ni changa sana kimaendeleo  hata ongezeko la watu lilikuwa ni chini tofauti na sasa ambapo tupo zaidi ya milioni 40.ongezeko hili linafanya uitaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo ya jamii yetu kuongezeka.
Katika suala la miundo mbinu ya nchi yetu ilikuwa duni sana lakini sasa tunaweza kushuhudia nchi yetu ikiunganishwa na mikoa mingi kwa kiwango cha rami.
Elimu,shule za msingi na sekondari zimeongeka na kuwezesha jamii kupeleka watoto wao shule ili kukabiliana adui ujinga.
 Elimu ya juu,vyuo vinavyotoa elimu ya juu vimeongezeka ili kusaidia watu kupata elimu ya juu tofauti na kabla ya uhuru vyuo vilivyotegemewa vilikuwa ni vya nje lakini sasa nashuhudia vyuo mbalimbali vikitoa wasomi wa fani tofauti kama wahandisi,walimu,wahasibu,waandishi wa habari  na matabibu na wengine wengi wakiongezeka Tanzania.
Kilimo,najivunia kuona kuwa miaka 52 jamii yetu imeweza kutambua sekta ya kilimo kwa kuanzisha sera ya kilimo kwanza ili kila mtu awajibike katika kilimo ili kujipatia kipato na chakula kwaajili ya kupambana na adui umasikini.
Afya,huduma za afya zimeongezeka sehemu mbalimbali ili jamii iweze kupata huduma ya afya kwa ukaribu.
Biashara,wajasiriamali wameongezeka,jamii imepata muamko wa kufanyabiasha za kitaifa na kimataifa katika kukabiliana na hali ya maisha kulinganisha na nyuma.
Ni mengi ambayo tunaweza kujivunia katika safari yetu ya miaka 52 ya uhuru kama nchi inayoendelea,tuangalie changamoto kama fursa kwetu na kuacha kujilinganisha na nchi nyingine ambazo zimeendelea siku nyingi.Naona Tanzania yetu inakua.
Mung Ibariki Tanzania


 

Jumapili, 8 Desemba 2013

Siku ya tatu katika kuomboleza Afrika kusini

Raia wa Afrika Kusini wako kwenye maombolezo kwa siku ya tatu hii leo ni siku maalum ya ibada na maombi maalum  kwa ajili ya kuomboleza mpendwa wao Kiongozi wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela, aliyeaga dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.







Ijumaa, 6 Desemba 2013

Hayati Nelson Mandela kuzikwa 15 december

Hayati Nelson Mandela anatarajiwa kuzikwa December 15 siku ya Jumapili mwaka huu katika eneo la Qunu Mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika kusini

FAHAMU NANI KUKUTANA NA NANI KATIKA KOMBE LA DUNIA MWAKANI

Cameroon wamejikuta katika kundi gumu la A pamoja na wenyeji Brazil, Mexico na Croatia.Mabingwa watetezi Uhispania watakuwa katika kundi B pamoja na Netherlands waliokutana nayo fainali kombe lililopita, na timu zingine ni Chile na Australia.
Dua ya Ivory Coast ya kuepuka kundi gumu sana wakati huu inaonekana imesikika, wako katika kundi C pamoja na Colomboa, Japan na Ugiriki.England watakuwa na kibarua kigumu kwenye kundi D ambapo wapinzani wao ni Italia, Uruguay na Costa Rica.
Kwenye kundi E Ufaransa inacheka usiku huu kwani imepangwa pamoja na Uswizi, Ecuador na Honduras.Mabingwa wa Afrika Nigeria wako katika kundi F pamoja na Argentina Iran na Bosnia Harcegovinia, ambayo inashiriki kombe la dunia mara ya kwanza.
Ghana ndiyo inayoonekana kuwa matatizoni miongoni mwa timu za Afrika. Wamejikuta katika kundi G ambapo watapamaba na na Ujerumani, Marekani na Ureno.Timu ya tano ya Afrika Algeria itakuwa kwenye kundi H na wapinzani hapo ni Ubelgji, Korea Kusini na Urusi

HISTORIA YA MWANAHARAKATI WA KWELI AFRIKA"NELSON MANDELA"

Nelson Mandela alizaliwa 18/7/1918 katika kijiji cha mvezo mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini.
Mandela jina lake la Nelson alipewa na mwalimu wake ambaye alishindwa kutaamka jina lake la Rolihlahla.
Akiwa kiongozi wa  chama cha ANC na mwanaharakati aliyetaka mabadiliko katika jamii ya watu weusi kwa kupata uhuru wa kujitawala wenyewe na kuondokana na ubaguzi wa rangi ulikuwa ukifanywa na watu weupe,alijikuta mara kwa mara akiwa katika misukosuko ya kukamatwa ambapo mwaka 1956 alikamatwa na wenzake 155 na kufunguliwa kesi ya uhaini kesi iliyochukua miaka 4 na kutupiwa mbali baada ya kukosa ushahidi wa kutosha.
Mwaka 1962 Mandela alikamatwa kwa kosa la kuondoka nchini bila kibali na 1964 alifungwa kifungo cha maisha katika kisiwa cha Robben.
Mnamo 1990      Rais FW De Klerk alimuachia huru mandela baada ya kukaa jela kwa miaka 27.
Mandela pia aliweza kupata tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya Amani Noble mwaka 1993.
Mnamo mwaka 1994 Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika kusini baada ya kufanyika uchaguzi ambao waafrika kusini walipiga kura zao.
Mandela aliweza kustafu urais baada ya miaka 5 ya uongozi wake .
Mwanzoni mwa mwaka huu Mandela alianza kuugua na kulazwa hospitali kwa muda wa miezi mitatu akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu,hali yake iliendelea vizuri na kuruhusiwa kutoka hospitali.

maisha ya Hayati Nelson Mandela kwa picha 1918-2013





Jumanne, 20 Agosti 2013

Floods in Manila




A woman wades in floodwaters brought by monsoon rain, intensified by tropical storm

Trami, in Kawit town of Cavite city, south of Manila August 19, 2013.

pictures




A Malaysian of Chinese ethnicity prays after burning joss paper money during Chinese Hungry Ghost Festival in Kuala Lumpur, August 19, 2013. The Hungry Ghost Festival is celebrated during the seventh month of the Chinese lunar calendar, when prayers are offered to the dead and offerings of food and paper-made models of items such as televisions, refrigerators and sport cars are burnt to appease wandering spirits. It is believed that the gates of hell are opened during the month and dead ancestors return to visit their relatives.

Jumatatu, 19 Agosti 2013

Asha Mandela, mwanamke mwenye nywele ndefu zaidi duniani.

"Kamwe sitokata nywele zangu"
Asha Mandela (50),mwanamke mwenye nywele ndefu duniani katika mtindo wa dread.
Mwanamke huyu anaamini kukata nywele zake ni sawa na kujiua.
Kumbe hata nywele zetu za kiafrika zinawezakuwa ndefu kama wale wenzetu,kweli inawezekana maana Bi.Asha ametudhihirishia hayo!
Mwanamke nywele!!!
source

Jumanne, 13 Agosti 2013

Woman attempts suicide by jumping off from high building in China.

Rescuers save a woman who was attempting suicide by jumping off a rainshed on the ninth floor of an apartment building, in Fuzhou, Fujian province, China, August 11, 2013. According to local media, the uninjured woman was rescued by firefighters and local residents after lying atop of the rainshed for over an hour.