Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambako Wakristo husheherekea kuzaliwa kwake Yesu
Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25Desemba
katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.
- Krismasi inatokana
na neno la kiingereza lenya maana "Christ`Mass" yaani misa au
ibada ya Kristo kwa maana misa ya sikuu yake.
Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokelewa na lugha ya Kifaransa "noël". Hili ni mafupisho ya Kilatini natalis (dies), "(siku) ya kuzaliwa Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu Utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.
Lakini baadaye
Ukristo ulienea katika Dola ya Roma na
kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo
ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo
asili ya Sikukuu ya Krismasi.
Tangu mwanzo wa
Karne ya 3BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya
kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Habari za
kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka
Misri mnamo mwaka 200.Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria alilalamikia
udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo
katika mwezi Mei wengine katika Aprili,Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo
cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa
kwake Yesu tarehe 6 Januari.
Labda kadirio
la tarehe ya 25 Desemba pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200 (kwa
mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Afrikanus tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri
tarehe 25 machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji
mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe
ya kuzaliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni