mashamba ya mfano mbogamboga kilimo hai ambacho hakitumii mbolea za chumvi,nananane 2013 Morogoro katika viwanja vya nanenane.
Kilimo cha
wakati huu ni tofauti na kilimo kilichokuwa kikitumiwa enzi za Ado Domino(AD)ambacho
kilikuwa kikitumia zana za kiasili katika kuzalisha,pia kilitumiwa kama shughuli ya kujipatia chakula
tu na bidhaa.
Kilimo karne hii
kimekuwa ni njia ya kukuza uchumi Dunia kwa sasa maana ni biashara,chakula,kinaendesha
sekta mbalimbali za usafirishaji,taasisi za fedha kama benki na viwanda ambavyo vimekuwa vikitegemea
malighafi kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hivyobasi mtazamo umekuwa chanya zaidi
katika jamii nyingi.
Kilimo hai(Organic
Farming) ni njia mbadala ya kumsaidia mkulima katika uzalishaji wake sababu
kinatumia gharama nafuu kwa malighafi zinazopatikana katika mazingira
yanayomzunguka na ni kilimo chenye mazingira rafiki na rahisi kumudu.
Kilimohai
kimekuwa kikitegemewa sana sababu kinazalisha mazao yenye ubora unastahili
kiafya na kimekuwa ni kilimo kinachotunza mazingira kwa matumizi endelevu na
yenye tija kwa mkulima.
Jamii nyingi za
Afrika hasa zimekuwa haziwekei mkazo kilimohai kama njia mbadala ya kuongeza
uzalishaji na utunzaji wa mazingira kwa kilimo endelevu kwa kutoweka kipumbele
cha kuelimisha umuhimu wa kutumia kilimo hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni