Jamii imekuwa ikilima mbogamboga kwa kutumia njia za kilimo hai,mboga hizo ni kama vile chinese, figiri, spinachi, spinachi chinese, saladi, tangawizi, viazi vitamu, kunde pia tuna alizeti, mtama na ufuta kwa ajili ya kuongeza uchumi wa jamii moja moja na Taifa kwa ujumla.
Kilimo cha mbogamboga ni muhimu kwa jamii hasa ya kitanzania popote anapoishi, awe kijijini au mjini. Haswa haswa wale wanaoishi mijini sehemu ambazo zina uhaba wa ardhi na ufinyu wa nafasi bila kuhitaji kuwa na ardhi na shamba kubwa.
Kutokana na kilimo cha mbogamboga mkulima anaweza mboga ambazo atatumia kwa matumizi yake mwenyewe,na kuongeza uchumi wake na Taifa kwa ujumla kwani anaweza kuboresha mboga zake na kuzikausha na kuuza kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu.
Happy peasant day(nanenane)!!1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni