Viongozi
wa serikali ya DRC wamehudhuria mazishi hayo huku waakilishi kutoka nchi jirani
ya Congo Brazaville pia wamehudhuria mazishi hayo.
Tabu
Ley alifariki mwezi Novemba akiwa na umri wa miaka 76 akipokea matibabu nchini
Ubelgiji.
Wengi
walimkumbuka Tabu Ley kwa mziki wake na kwa talanta yake kwa utunzi wa nyimbo
zake zilizowagusa watu wengi Afrika. Tabu Ley amefanyiwa mazishi ya kitaifa
Mwanamziki
huyo ambaye pia alikuwa mwanasiasa, hakuwahi kupona tangu alipougua kiharusi
mwaka 2008 na hali yake iliendelea kuwa mbaya hadi alipofariki Novemba 30.
Alizaliwa
mwaka 1937 katika kijiji kimoja kidogo Magharibi mwa mkoa wa Bandundu, na hapo
ndipo nyota yake ilianza kung'aa a katika fani ya muziki wa Rumba mapema miaka
ya sitini.
Baadhi
ya nyimbo alizoimba zilikuwa Adios Thethe na Mokolo nakokufa, na zilisaidia
katika kufanya mziki wa Rumba kupendwa sana.
Tabu
Lei alitaka sana kuwa waziri wa utamaduni katika serikali ya Laurent-Desire
Kabila --babake rais Joseph Kabila, lakini badala yake akawa naibu gavana wa
mji wa Kinshasa.
Alikimbilia
usalama wake wakati wa utawala wa aliyekuwa rais Mobutu Sese Seko kati ya mwaka
1965 to 1997, na mnamo mwaka 1990, serikali ya Mobutu ikapiga marufu album yake
Trop, c'est trop.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni