Tanzania imetimiza miaka 52 toka ipate uhuru wake kutoka kwa
waingereza walioyoitawala Tanganyika kama ilivyokuwa inajulikana wakati
huu kuanzia mwaka 1918-1961.
Ikiwa ni miaka 52 ya nchi yetu kujitawala yenyewe nashuhudia
mambo mbalimbali yanayoonyesha maendeleo japo tupo katika orodha ya nchini
zinazoendelea Dunia.
Maendeleo ni hali ya kutoka katika hali duni kuelekea katika
hali ambayo ni nzuri iwe kiuchumi,kisiasa na utamaduni.
Wakati tunapata uhuru 1961 nchi yetu ilikuwa ni changa sana
kimaendeleo hata ongezeko la watu
lilikuwa ni chini tofauti na sasa ambapo tupo zaidi ya milioni 40.ongezeko hili
linafanya uitaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo ya jamii yetu kuongezeka.
Katika suala la miundo mbinu ya nchi yetu ilikuwa duni sana
lakini sasa tunaweza kushuhudia nchi yetu ikiunganishwa na mikoa mingi kwa
kiwango cha rami.
Elimu,shule za msingi na sekondari zimeongeka na kuwezesha
jamii kupeleka watoto wao shule ili kukabiliana adui ujinga.
Elimu ya juu,vyuo vinavyotoa
elimu ya juu vimeongezeka ili kusaidia watu kupata elimu ya juu tofauti na
kabla ya uhuru vyuo vilivyotegemewa vilikuwa ni vya nje lakini sasa nashuhudia
vyuo mbalimbali vikitoa wasomi wa fani tofauti kama wahandisi,walimu,wahasibu,waandishi
wa habari na matabibu na wengine wengi wakiongezeka
Tanzania.
Kilimo,najivunia kuona kuwa miaka 52 jamii yetu imeweza
kutambua sekta ya kilimo kwa kuanzisha sera ya kilimo kwanza ili kila mtu
awajibike katika kilimo ili kujipatia kipato na chakula kwaajili ya kupambana
na adui umasikini.
Afya,huduma za afya zimeongezeka sehemu mbalimbali ili jamii
iweze kupata huduma ya afya kwa ukaribu.
Biashara,wajasiriamali wameongezeka,jamii imepata muamko wa
kufanyabiasha za kitaifa na kimataifa katika kukabiliana na hali ya maisha
kulinganisha na nyuma.
Ni mengi ambayo tunaweza kujivunia katika safari yetu ya
miaka 52 ya uhuru kama nchi inayoendelea,tuangalie changamoto kama fursa kwetu
na kuacha kujilinganisha na nchi nyingine ambazo zimeendelea siku nyingi.Naona
Tanzania yetu inakua.
Mung Ibariki Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni