Mwili
wa hayati Nelson Mandela umepelekwa katika mkoa wa Eastern Cape kwa safari ya
mwisho kabla ya kuzikwa siku ya Jumapili kijijini Qunu.
Idadi
kubwa ya watu walifurika barabara angalau kumtupia jicho shujaa wao na kutoa
heshima zao za mwisho.
Taarifa
zinazohusiana
Nelson
Mandela
Mandela
aliyefariki tarehe tano Disemba atafanyiwa maziko ya kitaifa siku ya Jumapili,
Takriban
watu 100,000 walitoa heshima zao za mwisho kwa Mandela mjini Pretoria siku ya
Ijumaa kabla ya mamia ya wengine kukosa fursa hiyo pale walipokatazwa kumuona
Mandela kutokana na ufupi wa mda.
Kijiji
cha Qunu
Kijiji
cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson Mandela, kinaomboleza kifo cha shujaa
aliyetoka katika kijiji hicho Nelson Mandela.
Mazingira
hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo
mfano wake ni mizinga ya Nyuki.
Visima
vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka hawezi kuviona sasa. Lakini viwanja
vya kijiji hiki viko chini ya majabali ambayo yeye na rafiki zake walikesha
wakichezea.
Ni
viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua asali misituni
na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo.
Alipokuwa
na umri wa miaka 5, Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu safari yake alivyopigania
uhuru wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga Ng’ombe, na kupitia kwa kazi
hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya watu wa kabila la AbaTembu na Ng’ombe
wao.
Alisomea
hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa huzuni wakati alimzika babake kimebadilika.
Lakini aliporejea hapa mwaka 1990 alipokuja kutembelea kaburi la mamake ,
alisema aliona umasikini mkubwa machoni mwa watu wa Qubu, viwanja visafi
alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa takataka kitu ambacho
hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.
Hata
hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka kimebadilika pakubwa, ni kisafi kikubwa na
kina dalili za maendeleo, wala sio taswira aliyoitoa Mandela katika kumbukumbu
zake kuhusu nyumbani.
Na
sababu moja ya hilo ni kuwa alijenga nyumba hapa pamoja na shule, alilemaji,
umeme, pamoja na mapato kwa watu wa eneo hili kutokana na makavazi aliyojengewa
Mandela ambako atazikwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni