Jumanne, 6 Agosti 2013

fashion and style

Nywele za asili ni nywele ambazo hazijawekwa kemikali ili kubadilisha uasili wake wa mwanzo.

Wanawake wa kiafrika wamekuwa na nywele za asili ambazo zikitengenezwa vizuri uonekana na mvuto wa kuvutia.

Kuwa na nywele za asili hakuna maana kwamba usibadilishe muonekano wako kwa rangi kama vile,rangi ya dhahabu,pink na nyeusi ya kung'aa.

Unaweza kutunza nywele za asili kwa kuziosha na shampoo na maji vuguvugu ili kusaidia kuondoa uchafu ulioganda katika nywele.

Kausha nywele kwa taulo,kitambaa kisafi au kwa "Dryer" mpaka uhakikishe hakuna maji kabisa yaliyobaki.Baada ya nywele kuwa kavu, paka mafuta ya kutosha kwenye nywele zako huku ukihakikisha ngozi nayo inapata mafuta kuepusha ukavu ambao mara nyingi husababisha mba.

Pia kuwa na nywele za asili kwa mwanamke hakumfanyi hasiwe na akiba ya wivin,rasta na wigs kwa ajili ya kubadilisha mitindo ya nywele mingine na inasaidia nywele kukua zaidi.

HIYO NI MITINDO MBALIMBALI YA NYWELE ZA ASILI,mwanamke nyweleeee

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni