Jumatatu, 5 Agosti 2013


mashamba ya mfano mbogamboga kilimo hai ambacho hakitumii mbolea za chumvi,nananane 2013 Morogoro katika viwanja vya nanenane.

Kilimo cha wakati huu ni tofauti na kilimo kilichokuwa kikitumiwa enzi za Ado Domino(AD)ambacho kilikuwa kikitumia zana za kiasili katika kuzalisha,pia  kilitumiwa kama shughuli ya kujipatia chakula tu na bidhaa.

Kilimo karne hii kimekuwa ni njia ya kukuza uchumi Dunia kwa sasa maana ni biashara,chakula,kinaendesha sekta mbalimbali za usafirishaji,taasisi za fedha kama benki na  viwanda ambavyo vimekuwa vikitegemea malighafi kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hivyobasi mtazamo umekuwa chanya zaidi katika jamii nyingi.

Kilimo hai(Organic Farming) ni njia mbadala ya kumsaidia mkulima katika uzalishaji wake sababu kinatumia gharama nafuu kwa malighafi zinazopatikana katika mazingira yanayomzunguka na ni kilimo chenye mazingira rafiki na rahisi kumudu.

Kilimohai kimekuwa kikitegemewa sana sababu kinazalisha mazao yenye ubora unastahili kiafya na kimekuwa ni kilimo kinachotunza mazingira kwa matumizi endelevu na yenye tija kwa mkulima.

Jamii nyingi za Afrika hasa zimekuwa haziwekei mkazo kilimohai kama njia mbadala ya kuongeza uzalishaji na utunzaji wa mazingira kwa kilimo endelevu kwa kutoweka kipumbele cha kuelimisha umuhimu wa kutumia kilimo hicho.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni