Jumanne, 24 Desemba 2013

Historia ya Krismas



 

Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu  ambako Wakristo husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.

 
Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii.

  • Krismasi inatokana na neno la kiingereza lenya maana "Christ`Mass" yaani misa au ibada ya Kristo kwa maana misa ya sikuu yake.

Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokelewa na lugha ya Kifaransa "noël". Hili ni mafupisho ya Kilatini natalis (dies), "(siku) ya kuzaliwa Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu Utamaduni  wa Wayahudi  wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.

Lakini baadaye Ukristo  ulienea katika Dola ya Roma na kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya Sikukuu ya Krismasi.

Tangu mwanzo wa Karne ya 3BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.

Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200.Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei wengine katika Aprili,Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.

Labda kadirio la tarehe ya 25 Desemba pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Afrikanus  tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni