Jumamosi, 28 Desemba 2013

Tips kwa mwaka mpya


Mwaka mpya unakuja kila mtu akiwa na malengo yake anayopenda Mungu amsaidie kuyatimiza. kutokana na sababu mbalimbali mtu hakuweza kutimiza maono yake kama kuwa mfanyakazi bora,kufaulu mitihani,kujenga nyumba au kuanzisha familia haijalishi vyote hivyo kama havikutimia katika mwaka uliopita sasa ni wakati wa kujipanga upya kwa mwaka ujao.Kuweka maazimio yetu,maono yetu na kumshirikisha Mungu  katika mwaka mpya wa 2014 itatusaidia kutimiza  ndoto tulizokuwa tukiota mwaka ulipita.. Tushirikiane hizi tips nne nilizopewa na rafiki yangu mpenzi miezi mitano iliyopita.

 
1. Kuanza kidogo: si vizuri kuanza kwa speed kubwa jipe muda wa kutosha ili kukamilisha kitu unachoanzisha,kuanzaa kidogo kutasaidia kujifunza taratibu na kukujengea uzoefu wa jinsi utakavyoweza kuhumudu kikubwa pindi kitakapoongezeka.Sio kukimbilia vikubwa ambavyo mwisho wa siku unalia kwa hasara au kushawishika na biashara haramu,kila kitu ni hatua kama vile mtoto anavyoanza kukaa,kutambaa,kusimama halafu hatua ya kutembea pole pole hadi mwisho wa siku ni mbio.


2. Kuwa na mlengo maalum : Unaweza kusema "Nataka kuanzisha biashara " au " Mimi nataka kupunguza uzito ," lakini unatakiwa kuweka azimio lako katika hali halisi itasaidia kweli kufikia lengo lako. Kwa mfano, jaribu kutatua kwa kujifunza jinsi ya kucheza wimbo maalum juu ya gitaa. Pia jaribu kuweka katika maandishi ili kusaiidia lengo kuwa halisi kufanyia kazi.


3. Jipe kikomo cha muda: Katika hili mtu anatakiwa ajiwekee kikomo cha kutekeleza malengo yake mfano, " Ningependa kuwa na biashara,anza kidogo kidogo utasogea lakini sio nafikiria kuanzisha biashara  siku moja hapo kamwe haitotokea,unachotakiwa ni kuchukua mara moja na kutekeleza adhima yako ya kuacha.pia na kuweka kikomo cha muda kuwa labda baada ya miezi mingapi biashara yako itakuweje.

.
4. Kuweka rekodi ya maendeleo yako: hii itakusaidia kukupa Ramani   jinsi ya kutunza azimio lako na kukufanya kufikia malengo yako.Hakuna hisia bora kuliko kuwa na lengo na kulikamilisha.Pia itakusaidia kujua wapi ulipofikia toka ulipoanza shughuli yako,iwe umeajiriwa au umejiajiri.

  

Pia tusisahau kuandika katika kumbukumbu zetu vitu tunavyotaka kuvifanya kwa mwaka mpya hii itatusaidia kutupa nguvu ya kufanya bidii katika malengo yetu na hatimaye kutimiza ndoto zetu.

Mwaka mpya mwema wenye Baraka na mafanikio,Mungu awabariki.

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni