Ijumaa, 6 Desemba 2013

HISTORIA YA MWANAHARAKATI WA KWELI AFRIKA"NELSON MANDELA"

Nelson Mandela alizaliwa 18/7/1918 katika kijiji cha mvezo mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini.
Mandela jina lake la Nelson alipewa na mwalimu wake ambaye alishindwa kutaamka jina lake la Rolihlahla.
Akiwa kiongozi wa  chama cha ANC na mwanaharakati aliyetaka mabadiliko katika jamii ya watu weusi kwa kupata uhuru wa kujitawala wenyewe na kuondokana na ubaguzi wa rangi ulikuwa ukifanywa na watu weupe,alijikuta mara kwa mara akiwa katika misukosuko ya kukamatwa ambapo mwaka 1956 alikamatwa na wenzake 155 na kufunguliwa kesi ya uhaini kesi iliyochukua miaka 4 na kutupiwa mbali baada ya kukosa ushahidi wa kutosha.
Mwaka 1962 Mandela alikamatwa kwa kosa la kuondoka nchini bila kibali na 1964 alifungwa kifungo cha maisha katika kisiwa cha Robben.
Mnamo 1990      Rais FW De Klerk alimuachia huru mandela baada ya kukaa jela kwa miaka 27.
Mandela pia aliweza kupata tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya Amani Noble mwaka 1993.
Mnamo mwaka 1994 Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika kusini baada ya kufanyika uchaguzi ambao waafrika kusini walipiga kura zao.
Mandela aliweza kustafu urais baada ya miaka 5 ya uongozi wake .
Mwanzoni mwa mwaka huu Mandela alianza kuugua na kulazwa hospitali kwa muda wa miezi mitatu akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu,hali yake iliendelea vizuri na kuruhusiwa kutoka hospitali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni